Pata taarifa kuu

Waislamu wajiandalia mfungo wa mwezi wa Ramadhani

Waislamu kote ulimwenguni wanaanza ibada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Jumanne wiki hii, katikati ya sintofahamu inayotokana na hatua za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona ambazo ni pamoja na kuwazuia watu usafiri n kutotoka nje katika baadhi ya nchi.

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan waanza kwa Waislamu. Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa kusoma sana Q'uran.
Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan waanza kwa Waislamu. Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa kusoma sana Q'uran. © SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Virusi vya corona kwa kiasi kikubwa vimebadilisha mfumo wa Maisha duniani, huku mataifa yakipambana kwa kila hali kukabiliana na maradhi yanayosababishwa na virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Karibu vifo Milioni 2.94 vimetokea duniani kote kutokana na ugonjwa huo, idadi ya walioambukizwa hivi sasa inakaribia milioni Milioni 136, na pia uchumi wa dunia umeathirika pakubwa.

Waumini wa dini ya Kiislamu kuanzia Kusini Mashariki mwa Asia hadi Mashariki ya Kati na hata Afrika wanaanza mwezi huu mtukufu katikati kadhia ya mapambano haya, kwa kuzuiwa kukusanyika na hata kutoka nje katika baadhiya nchi.

Ubora wa mwezi mtukufu wa Ramadhan

Katika kipindi cha siku 29 au 30 Waislam hujizuwiya kula na kunywa kuanzia alfajiri hadi jua linapozama takriban siku 30 au 29 kutegemea na muandamo wa mwezi.

Mwezi wa Ramadhani ni moja ya miezi mitukufu katika kalrenda ya kiislamu ambao husubiri kwa hamu kubwa na waumni wote wa kiislamu ulimwenguni.

 Mwezi wa Ramdhani ni mwezi wa kuzidisha upendo, kutoa sadaka na kuwakumbuka wote wale wenye kuhitaji msaada.

Ramadhan huanza mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislam ambapo Waislam wanaamini Kuran Takatifu iliwasilishwa kwa Mtume Mohammad katika karne ya saba mnamo mwezi wa Ramadhan.

Waislamu wanaamini kuwa huu ni mwezi wa kupatiwa msamaha na Mwenye-Enzi-Mungu kwa hiyo huzidisha ibada kwa wingi na kuwa karibu na Mwenye-Enzi-Mungu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.