Pata taarifa kuu
WHO

COVID-19 bado ni tishio duniani

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya Duniani, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema katika mkutano na waandishi wa habari wakati anatoa tamko la dharura ya afya ya umma duniani ambalo ni onyo la ngazi ya juu zaidi chini ya sheria ya kimataifa, kulikuwa na wagonjwa wasiozidi Milioni 100 na hakukuweko na kifo chochote cha COVID-19 nje ya China.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus Fabrice Coffrini/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

“Kuelekea mwaka mmoja tangu ugonjwa wa Corona au COVID-19 utangazwe kuwa dharura ya afya ya umma duniani, bado ugonjwa huo umesalia kuwa hatari na kutishia siyo tu nchi maskini bali pia tajiri” , amesema Dkt. Tedros Ghebreyesus.

“Wiki hii, tumefikia wagonjwa Milioni 100. Wagonjwa wengi zaidi wameripotiwa wiki mbili zilizopita kuliko wiki 6 za mwanzo za janga hili. Mwaka mmoja uliopita nilisema kuna fursa ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi hivi, baadhi ya nchi ziliitikia wito na baadhi hazikuitikia,” ameongeza Dkt. Tedros.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa WHO amesema ingawa hivyo baadhi ya nchi hazikuitikia wito wake wa mwaka jana, sasa kuna fursa nyingine kupitia chanjo ya COVID-19 ambayo inaweza kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo. “Tusipoteze fursa hii.”

Dkt. Tedros ametaja suala la uzawa kwenye chanjo ambalo linaweza kukidhi tu mahitaji ya muda mfupi ya kisiasa ambayo yatakuwa na madhara siku za baadaye akisema kuwa, “hatuwezi kumaliza janga hili pahala fulani bila kulimaliza kila pahala.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.