Pata taarifa kuu
WHO

WHO yaendelea kukutana kwa mazungumzo na wanasayasi kuhusu mlipiuko wa COVID-19 Wuhan

Ndugu za watu ambao wamekufa kutokana na virusi vya Corona nchini China wanadai kukutana na timu ya wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyoko huko Wuhan kuchunguza asili ya virusi hivyo, wakisema serikali ya China imeshindwa kuwapa majibu kamili dhidi ya madai yao.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Licha ya China kuwakubalia wataalamu hao wa WHO kwenda Wuhan, haijafahamika iwapo watapata nafasi ya kuzungumza na familia za watu waliokufa kutokana na Corona, wakati huu wakiendelea kuzungumza na wanasayansi kuhusu kiini cha virusi hivi.

Virusi vipya vya Corona (COVID-19) viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China. Hivi ni virusi vipya vya korona ambavyo havijatambuliwa hapo awali kwa wanadamu.

Virusi vya Corona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS).

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.