Pata taarifa kuu
WHO-CHANJO

WHO yasema dunia inakabiliwa na utovu wa maadilu kuhusu chanjo

Shirika la afya duniani WHO linaonya kuwa dunia inakabiliwa na utovu wa maadili kuhusu namna ugawaji wa chanjo ya kuzuia virusi vya Corona, unavyofanyika.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema inasikitisha kuwa, vijana wenye afya kutoka mataifa tajiri wanapata chanjo, huku wazee wasiojiweza kwenye nchi masikini duniani, wkaiendelea kuhangaika.

Hadi sasa, dozi Milioni 39 za chanjo zimetolewa kwa nchi tajiri zipatazo 49 ikilinganisha na Dozi 25 kwa taifa moja masikini.

Mpaka sasa nchi za China, India, Urusi , Uingreza na Marekani zimefanikiwa kutzngeza chanjo za kuzuia mamabukizi ya corona pamoja na kampuni ya Marekani na Ujerumani Pfizer.

Katika hatu nyingine, WHO na China, zinaendelea kulaumiwa  kwa kushindwa kuzuia kusambaa maambukizi ya corona mapema kwa mujibu wa ripoti ya watalaam walioteuliwa na Shirika hilo, kuchunguza namna maambukizi hayo yalivyosambaa.

Kote duniani, wakati chanjo zinapoendelea kutolewa, watu zaidia ya Milioni 95.5 wameambukizwa huku wengine zaidi ya Milioni 2.04 wakiripotiwa kupoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.