Pata taarifa kuu
UBELGIJI-UFARANSA-UGAIDI

Assia: "sikujua kuwa alikua anatafutwa"

Assia anasema, wakati alikubali kumpokea na kumpa hifadhi mtu aliekutana naye katika mgahawa, Aprili 5, hakujua kabisa kuwa ni Mohamed Abrini, mtuhumiwa wa mashambulizi ya mjini Paris na Brussels, na alikua akitafutwa na polisi zote za Ulaya.

Viwambo kutoka kamera za CCTV za uwanja wa ndege wa Brussels, zikionyesha "mtu mwenye kofia," Mohamed Abrini, mtuhumiwa wa tatu wa mashambulizi ya mjini Brussels.
Viwambo kutoka kamera za CCTV za uwanja wa ndege wa Brussels, zikionyesha "mtu mwenye kofia," Mohamed Abrini, mtuhumiwa wa tatu wa mashambulizi ya mjini Brussels. REUTERS/CCTV/Belgian Federal Police/
Matangazo ya kibiashara

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 43, aliachiliwa huru siku mbili baada ya kuzuiliwa nyumbani kwake. Alizuiliwa nyumbani kwake baada ya Mohamed Abrini kukamatwa. Assia aliposikilizwa na majaji, alisema hakuweza kumtambua Mohamed Abrini.

"Kijana tu kama hivi, siningeweza kuwa na mashaka naye kwamba ni mtu anayetafutwa," Assia ameiambia runinga ya BFM TV. "Alikuwa mtu wa kawaida. Labda alikua ameficha tabia yake. Katika siku mbili, huwezi kumjua mtu."

Mohamed Abrini alikua na Fedha nyingi

Mohamed Abrini alibaki usiku mmoja na nyumbani kwake, Assia amesema. Kwa mujibu wa Assia, Abrini aliweza kumwambia kuwa alisahau kadi yake ya uraia kwa wazazi wake, ambao walikuwa nchini Ujerumani. Maelezo mengine muhimu, kijana huyo alionekana kuwa na fedha nyingi. "Alikuwa na fedha, fedha nyingi hasa, Assia anakumbuka. Alikuwa na pesa nyingi za 50 na za 20."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.