Pata taarifa kuu
INDONESIA-Siasa

Indonesia: Joko Widodo aapishwa kuwa rais

Rais mpya wa Indonesia ameapishwa leo Jumatatu Oktoba 20, ikiwa ni miezi mitatu baada ya kuchaguliwa kwenye wadhifa huo. Indonesia inaundwa na visiwa 13,466 ambavyo vina wakaazi milioni 240. Asilimia 90 ya raia wa Indonesia ni Waislam.

Rais mpya wa Indonesia, Joko Widodo (katikati), wakati wa kuapishwa kwake, Oktoba 20 mwaka 2014, Jakarta.
Rais mpya wa Indonesia, Joko Widodo (katikati), wakati wa kuapishwa kwake, Oktoba 20 mwaka 2014, Jakarta. REUTERS/Darren Whiteside
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Jerry amewasili nchini Indonesia leo Jumatatu kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais Joko Widodo na kuchochea mataifa ya Kusini mwa Asia kupiga hatua katika jitihada zao za kupambana na kundi la Islamic State.

Kerry ni miongoni mwa vigogo wa kigeni wanaozuru Jakarta kushuhudia kuapishwa kwa Widodo,mfanyabiashara wa zamani wa ambaye ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya wanasiasa wasomi na jeshi.

Wakati wa ziara yake ya siku moja, Kerry atatumia mfululizo wa mikutano ya nchi na nchi kumwomba Widodo, na viongozi wengine wa Kusini mwa Asia kuchukua hatua zaidi dhidi ya tishio linaloongezeka kutoka kundi la Islamic State maafisa wamesema.

Joko Widodo atajaribu kuleta mabadiliko katika taifa hilo la kwanza kiuchumi katika Asia ya Kusini.

Asilimia kubwa ya raia wa Indonesia wana imani kwamba rais huyo ataleta mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali.

Tangu mwaka 1998 na baada ya kutimuliwa kwa utawala wa kiimla wa dikteka Suharto, aliye ongoza taifa la Indonesia kwa muda wa miaka 32, marais waliyofuta waliku ni kutoka katika Ukoo wa dikteta huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.