Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-Maandamano-Siasa

Hong Kong: Polisi yaondoa vizuizi barabarani

Hali ya taharuki imeendelea kutanda katika mji wa Hong Kong, nchini china licha kumchakato wa mazungumzo uliyoanza hivi karibuni kusitishwa. Baada ya maandamano makubwa yaliyofanyika Ijumaa jioni wiki iliyopita.

Polisi yaondoa vizuizi katika mitaa ya mji wa Admiralty, Oktoba 13 mwaka 2014.
Polisi yaondoa vizuizi katika mitaa ya mji wa Admiralty, Oktoba 13 mwaka 2014. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu wa Leung Chun-ying ameongea kwenye televisheni ya taifa akiwataka waandamaniji hao wasitishe maandamano hayo.
Tangu asubuhi Jumatatu wiki hii polisi imekua ikiondoa vizuizi wiliyowekwa na waandamanaji kwenye barabara tofauti za mji wa Hong Kong

Vuguvugu la watu wa miavuli wanaandamana kwa siku ya 16 leo Jumatatu, huku wakiendelea kushikilia mji mitatu. Hata hivo polisi imekua ikijaribu kuondoa vizuizi viliyowekwa kwenye barabara za maeneo ambayo hayajadhibitiwa na waandamanaji hao. Katika maeneo mengi polisi imekua ikiondoa vizuizi hivyo bila upinzani wowote.

Katika eneo la kibiashara la Mongkok ambalo lilikua kama eneo muhimu la waandamanaji, polisi ilijaribu kuongea na waandamanaji kwa muda wa dakika 45, na baadaye waandamanaji walikubali kusalimu amri ya kuondoka..

Wakati huo huo, idadi ya polisi imeendelea kuongezwa katika mji wa Admiralty. Askari polisi wamekua wakivalia nguo zao za kawaida wala siyo sare yao wanaoivaa kwa kukabiliana na makundi ya wahuni.

Hata hivo polisiimekua ikiwaondoa baadhi ya waandamannaji waliolalala katika barabara za mji wa Hong Kong kuendelea kushinikiza mabadiliko ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2017.

Mahema yaliyokuwa yamejengwa na waandamanaji hao yameondolewa ili kuruhusu shughuli za kawaida kurejea katika mji huo wa kiuchumi kwa China.
Mwishoni mwa juma lililopita, viongozi wa Hong Kong walisema shinikizo za waandamanaji hao haziwezi kuzaa matunda yoyote.

Waadamanaji hao wanataka China kutoingilia maswala ya siasa katiaka eneo hilo wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.