Pata taarifa kuu
Syria-Diplomasia

Takriban wapiganaji 17 wa makundi ya kiislam wapoteza maisha katika shambulio la jeshi la serikali likishirikiana na Hezbollah

Takriban wapiganaji 17 wa makundi ya kiislam wamepotwza maisha jana katika mapigano na jeshi la serikali linaloshirikiana na kundi la Hezbollah katika harakati za kuukomboa mji wa Yabroud. Jeshi la Anga limeendesha mashambulizi mapema ijumaa hii katika ngome za wapiganaji wenye mafungamano na kumdoi la Alqaeda waliojificha karibu na mji wa Yabroud. 

Vifaru vya jeshi la Syria
Vifaru vya jeshi la Syria
Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya ambayo Kundi la Kishia la Hezbollah linahusika moja kwa moja yanalenga kuzuia upenyaji wa aina yoyote kuelekea nchini Lwbanon hususan kupitia katika mji wenye waumini wengi wa kisunni Aarsal katika bonfe la Bekaa.
Kundi la Hezbollah linasema gari zinazo lipuka zikilenga ngome za Hezbollah hutegwa bomu kutokea katika mji huo wa Yabroud kabla ya kuelekea nchini Lebanon kutokea Aarsal

Katika hatuwa nyingine, wataalam wa mizozo na siasa za kimataifa wameonya kuwa mzozo wa syria huenda ukadumu kwa miaka kumi zaidi ijayo ikiwa Iran na Urusi zitaendelea kuuunga mkono utawala wa raisi wa syria Bashar al asssad na kundi la wapiganaji wa kijihad wanaoendesha mapigano nchini humo.

Wachambuzi hao wanaona kuwa Rais Assad ametumia njia ya kushirikiana na wapiganaji kama al-Nusra na taifa la kiislamu la Iraq dhidi ya wapinzani wenye msimamo mkali wanaoungwa mkono na Marekani.

Wataalam hao wanasema Kwa sasa inaonekana kuanguka kwa utawala wa Assad sio jambo rahisi kama wachambuzi wengi walivyoamini mwaka uliopita akinukuu baadhi ya wachamuzi kutoka Marekani ambao waliona kuwa siku za raisi Assad kusalia madarakani zinahesabika.

Kwa sasa hata Jumuiya ya intelijensia ya Marekani inaona kuwa vita huenda ukaendelea kwa muongommoja zaidi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.