Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAUAJI

Boko Haram watekeleza mauaji ya watu zaidi ya hamsini kaskazini mwa Nigeria

Wanamgambo wa kundi la  Boko Haram nchini Nigeria wamewaua zaidi ya watu 50 kwa kuwapiga risasi katika jimbo la Maiduguri Kaskazini mwa nchi hiyo. Hii ikiw ana muendelezo wa mashambulizi ya yanayo tekelezwa na kundi hilo kaskazini mwa nchi hiyo tangu kipindi kadhaa.

Wanamgambo wa kundi la Boko Haram
Wanamgambo wa kundi la Boko Haram
Matangazo ya kibiashara

Inaripotiwa kuwa wanamgambo hao pia waliteketeza moto maakazi ya watu katika kijiji cha Mainok na baadaye kutekeleza mashambulizi kadhaa ya mabomu.

Mashambulzi haya yalitokea siku ya Jumapili iliyopita na kuendelea kusabaisha hali ya wasiwasi kuwakumba wenyeji wa Maeneo ya Kaskazini mwa taifa kutokana na kuendelea kwa mashambulizi haya ambayo yamekuwa yakiendelea kwa mwaka wa nne sasa.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan juma lililopita alisema kuwa jeshi linafanya kila kilicho ndani ya uwezo wao kulitokomeza kundi hilo na kufikia mwezi Mei mwaka huu, wanagambo wa Boko Haram watakuwa wametokomezwa.

Ufaransa imeahidi kuisaidi Nigeria kupambana na kundi hilo ambalo limetekleza mauji ya maelfu ya watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.