Pata taarifa kuu
VENEZUELA-Maandamano

Maandamano yashika kasi nchini Venezuela

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Venezuela, ambao wanaandamana kwa muda wa majuma matatu dhidi ya utawala wa rais Nicolas Maduro wameweka viziwizi kwenye barabara kuu zinazoingia katikati ya mji wa caracas, ikiwa ni hatua ya juu kutekelezwa na waandamanaji hao toka walipoanza harakati zao.

Waandamanaji wakijaribu kuweka viziwizi kwenye barabara za mji wa Caracas, nchini Venezuela.
Waandamanaji wakijaribu kuweka viziwizi kwenye barabara za mji wa Caracas, nchini Venezuela. RAUL ARBOLEDA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yanaendelea, wakati serikali ilianza kukutana tangu jumamosi na wadau wote, ili kuanzisaha mazungumzo ya kitaifa.

Rais Nicolas Maduro, madarakani kwa muda wa miezi 11, anakabiliwa na maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu wakiungwa mkono na upinzani tangu mwanzoni mwa mwezi wa februari dhidi ya usalama na maisha duni.

Kulingana na takwimu rasmi, na idadi inayotolewa na shirika la habari la AFP, watu 14 wameshapoteza maisha, wakiwemo wanane ambao waliuawa kwa kupigwa risase, na wengine 140 wamejeruhiwa tangu maadamano hayo yalipoanza.

Moshi mkubwa wa uliotokana na kuchomwa kwa matairi ya gari ulitanda kwenye mji wa Andes na Caribbean kuongeza shinikizo zaidi kwa serikali ya Rais Nicolas Maduri ambayo imeendelea kutia ngumu kutekeleza madai ya waandamanaji hao.

Katika hatua nyingine, upinzani nchini humo umekataa kushiriki kwenye mazungumzo yaliyoitishwa na rais Maduro hapo kesho wakisisitiza kwanza kuachiliwa kwa viongozi wa kisiasa wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama.

Rais Maduro anasema huu ni mpango wa mataifa ya magharibi kutaka kuipindua Serikali yake.

Mwanamuziki maarufu kutoka Colombia, Shakira, ambaye yuko ziarani mjini Carthagène, nchini Colombia, amesema ana imani kuwa amani itarejea haraka nchini Venezuela, raia wa nchi hiyo watakua katika amani ya kudumu.

Kundi la waandamanaji liliweka viziwizi vingi jana katika mji wa Caracas, ili kuziwiya makabiliano na vyombo vya usalama, na hali hio ilisababisha waedesha baskeli na pikipiki kuwa na hasira, wameshuhudia waandishi wa AFP.

Katika miji mingine, kama Valencia, mji wa tatu kwa ukubwa nchini Venezuela, kulitokea machafuko yaliyosababishwa na makabiliano kati ya waandamanaji na polisi, ambao walilazimika kufyatua risase za plastiki na mabomu ya kutoa machozi dhidi ya vijana waliyokua waliweka viziwizi kwenye barabara inayoelekea mjini.

Nicolas Maduro, mrithi wa kisiasa wa Hugo Chavez (katika miaka ya 1999-2013), ambaye alifariki kutokana na maradhi ya saratani machi 5 mwaka 2013, amekua akinyooshea kidole cha lawama Marekani kwamba imekua ikiunga mkono upinzani ili uendeleye na machafuko hayo.

Maduro amesema maadui wa taifa hilo, wameamua kuzua fujo ili waipinduwe serikali yake.

Katika tangazo liliyorushwa hewani kwenye vyombo vya serikali jana jumatatu, Maduro, amesema kwamba wamemkamata Jayssam Mokded, anayedaiwa kwamba “ni mamluki kutoka mashariki ya kati”, ambaye amekua akiandaa mashambulizi ya kujilipua.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.