Pata taarifa kuu
KUWAIT

Viongozi wa mataifa ya kiarabu wakutana nchini Kuwait kujadili mipango ya kuongeza ushirikiano

Viongozi wa mataifa ya kiarabu yenye utajiri kwa mafuta wanakutana nchini Kuwait leo Jumanne kujadili mipango ya kuongeza ushirikiano wakati wa tofauti kuhusu mapendekezo ya muungano na mahusiano ya karibu na Iran. 

Waziri wa mambo ya kigeni wa Oman Yussef bin Alawi
Waziri wa mambo ya kigeni wa Oman Yussef bin Alawi NOAA/AFP/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa nje wa mataifa sita ya muungano wa Baraza la Ushirikiano wa Ghuba(GCC) jana Jumatatu walikamilisha ajenda ya mwisho kwa mkutano wa siku mbili, ambayo pia itashughulikia mgogoro wa Syria.

Mkutano huo wa kilele unafuatia malumbano nadra ya umma kati ya kiongozi wa kanda Saudi Arabia na Oman kuhusu pendekezo la Riyadh la kuipandisha GCC kuwa muungano, miaka 32 baada ya kuanzishwa kwake.

Omani Waziri wa mambo ya nje wa Omani Yussef bin Alawi alitishia kwamba Muscat itajiondoa kwenye muungano huo unaotetereka ikiwa muungano utatangazwa, wakati Saudi Arabia ikiungwa mkono kwa dhati na Bahrain ilisisitiza kuwa ni wakati wa kusonga mbele.

Waziri wa nchi anayeshughulikia baraza la mawiziri nchini Kuwait Sheikh Mohammad Abdullah Al-Sabah, hata hivyo amewaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo kuhusu muungano yataendelea.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.