Pata taarifa kuu
CHILE

Rais wa zamani wa Chile, Michelle Bachelet ang'ara katika matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu

Rais wa zamani wa Chile, Michelle Bachelet ameibuka na ushindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika jana jumapili. Michelle ameibuka kinara dhidi ya mpinzani wake Evleyn Matthei wa chama cha kiliberali, hata hivyo itabidi wawili hao wachuane katika duru ya pili ya uchaguzi itakayoganyika tarehe 15 mwezi ujao kutokana na wote kushindwa kufikisha asilimia 50 ya kura zote.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Bachelet ambaye ni mwanamke wa kwanza kuwa Rais nchini humo na amejipatia zaidi ya asilimia 47 dhidi ya mpizani wake Evleyn Matthei ambaye aliyeambulia asilimia 25 ya kura zote.

Bachelet ambaye ni Daktari wa watoto kutoka chama cha kisocialist na alikuwa rais wa Taifa hilo mwaka 2006 hadi 2010 aliondoka madarakani na nafasi yake kuchukuliwa na Sebastian Pinera.

Bachelet alikwenda kuhudumu katika Umoja wa Mataifa UN baada ya kuondoka madarakani, na kurejea nchini mwake mwanzoni mwa mwaka huu na kudai kuwa bado kuna mambo mengi ya kufanya nchini mwake.

Takriban wananchi milioni 13.5 wamepiga kura jana na kuamuwa kumrejesha madarakani Rais huyo wa zamani ambaye alikuwa bado anaushawishi mkubwa nchini mwake.

Wagombea wote wawili ni wanawake, na watoto wa viongozi zamani wa kijeshi nchini huno na ambapo baba ya mpinzani wa Michelle Bachelet Evleyn Matthei alikuwa mshirika wa karibu wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo AugustoPinochet na ambapo Bachelet ametumia karata hiyo katika kunadi sera zake wakati wa kampeni za uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.