Tuzo ya amani ya Mo Ibrahim imekosa mshindi kwa mara nyingine tena
Tuzo la Mo Ibrahim, ambalo hutolewa kwa viongozi wastaafu waliohudumu kwa kuheshimu sheria na utawala bora, imekosa mshindi kwa mwaka wa nne sasa tangu kuundwa kwake miaka saba iliopita.
Imechapishwa:
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini London, wakfu wa Mo Ibrahim umesema kuwa baada ya kutafakari kwa makini, wamemkosa mshindi wa tuzo hiyo mwaka huu wa 2013.
tuzo hiyo ya Mo Ibrahim hutolewa kwa kiongozi aliye teuliwa katika misingi ya kidemokrasia na amabye amestaafu kwa kipindi cha miaka mitatu, na ambaye uongozi wake uliheshimu sheria na misingi ya utawala bora.
Tuzo hiyo ilianzishwa na mfanyabiashara bilionea raia wa Uingerwza mwenye asili ya Sudan, Mo Ibrahim hutoa dola milioni 5 kwa kipindi cha miaka kumi na dola laki mbili kila mwaka hadi kiongozi huyo atakapofariki.
Mbali na kitita hicho dola laki mbili hutolewa kwa mradi wowote unaoungwa mkono na mshindi wa tuzo hiyo kwa kipindi cha miaka kumi.
Huu umekuwa ni mwaka wa nne tuzo hiyo inakosa mshindi tangu kuanzishwa kwake miaka 7 iliopita. Mtu wa kwanza kupewa tuzo hiyo alikuwa ni Joachim Chisano rais mstaafu wa Msumbiji, mwaka 1995, Festus Mogae wa Botswana 2008 pamoja na
Pedro Pires wa Cape Verde mwaka 2011.