Pata taarifa kuu
Korea kaskazini

Mazungumzo ya Korea Kaskazini na Kusini yamalizika bila kufikia Muafaka

Korea kusini imesema kuwa Mazungumzo na Korea kaskazini juu ya kufungua tena eneo la viwanda yamemalizika bila kufikia makubaliano, lakini pande hizo mbili zimekubaliana kukutana tena juma lijalo.

Eneo la Viwanda vya Kaesong lililo Korea kaskazini
Eneo la Viwanda vya Kaesong lililo Korea kaskazini
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Ujumbe wa Korea kusini, Suh Ho amesema Mazungumzo juu ya kufunguliwa tena kwa eneo la viwanda la Kaesong yataendelea tarehe 15 mwezi huu baada ya Saa kadhaa za Mazungumzo yaliyoanza jana asubuhi.
 

Mazungumzo yamekuja baada ya msuguano baina ya pande mbili na tishio la Pyongyang kuingia vitani baada ya Jaribio lake la Nuklia lililosababisha kuwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa vilivyofanya Korea kaskazini kuyumba kiuchumi.
 

Eneo la viwanda la Kaesong lilifungwa miezi mitatu iliyopita baada ya mzozo wa majirani hao kupamba moto.
 

Lakini Mazungumzo yao juu ya kufunguliwa tena kwa eneo hilo, kunatoa ishara ya kufikiwa kwa Maridhiano baina ya Korea kaskazini na Kusini.
 

Wamiliki wa kiwanda kutoka Korea kusini, waliotembelea maeneo yao ya kiwanda wakati mazungumzo yakiendelea wamesema kuwa baadhi ya vifaa vimeharibika na kutu na kuongeza kuwa kufungwa kwa eneo la Viwanda kulimaanisha kuwa Biashara katika eneo hilo ingekufa kabisa.
 

Wafanya biasdhara hao wamesema wanaona kuwa wasifungue tena Viwanda mpaka pale Korea kaskazini itakapoahidi kuwa hali yaliyotokea hayatajirudia tena.
 

Eneo la viwanda vya Kaesong, lilijengwa mwaka 2004 nchini Korea Kaskazini, sehemu ya eneo hili likiwa limewekezwa na Korea kusini zikiwa ni jitihada za mahusiano mazuri ya kidiplomasia baina ya nchi hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.