Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI-MAREKANI

Serikali ya Afghanistani yatishia kususia mazungumzo ya amani kati yake na Taliban

Serikali ya Afghanistan imetishia kugomea mazungumzo ya amani yaliyopangwa kati yake na Wanamgambo wa Taliban, mazungumzo yaliyopangwa kufanyika nchini Qatar ikisema kuwa sharti mazungumzo hayo yaongozwe na Afghanistani.

Rais wa Afghanistani Hamid Karzai
Rais wa Afghanistani Hamid Karzai REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zimesema kuwa Hatua ya sasa inaonesha kuwa kuna mikono ya nje ambayo iko nyuma ya Taliban hivyo hawatashiriki mpaka pale Afghanistani itakapoongoza mazungumzo hayo.
 

Serikali ya nchi hiyo pia imekosoa Kujihusisha kwa Marekani katika makubaliano ya kufungua Ofisi ya kundi la Wanamgambo wa Taliban nchini Qatar kwa ajili ya kuratibu Mazungumzo ya amani.
 

Rais wa Afghanistani, Hamid Karzai alivunja mazungumzo kuhusu maswala ya usalama yaliyokuwa yafanyike kati ya Afghanistani na Marekani, kutokana na kukasirishwa na jina lililotolewa la Ofisi za Taliban nchini Qatar.
 

Ofisi za Taliban nchini Qatar zimepewa jina la Islamic Emirate of Afghanistan, jina la zamani la Chama cha kiislamu kilichokuwa kikitawala mwaka 1996 mpaka Serikali ya Chama hicho ilipoangushwa mwaka 2001.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.