Pata taarifa kuu
Marekani

Marekani kutoiondoa Cuba kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetangaza kwamba haina mpango wowote wa kuliondowa taifa la Cuba kwenye orodha ya nchi zinazo tuhumiwa kuunga mkono Ugaidi, kama ilivyo kwa Syria, Iran, Sudan.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Naibu msemaji wa wizara Patrick Ventell amesema hakuna mpango wowote wa mabadiliko katika orodha hiyo ya nchi zinazounga mkono ugaidi, na hakuna nia ya kuiondowa Cuba katika orodha.

Wizara hiyo ya mambo ya nje ya Marekani imekuwa ikitagaza orodha kila mwaka ya nchi na mashirika yanayo unga mkono ugaidi, ripoti ambayo hutolewa kila April 30, lakini mwaka huu ripoti jhiyo imeahirishwa kutolewa na huenda ikawekwa kabla ya mwezi huu wa Mei kumalizika.

Wakati huohuo Wanaharakati kutoka Jumuia ya Kimataifa wametoa wito kwa Marekani kuheshimu na kuhakikisha Wafungwa wa gereza ya guantanamo wanapata haki yao ya kuishi, huduma za afya,na haki nyingine za msingi.
 

Wanaharakati wametoa wito huo baada ya kuripotiwa kuwa takriban Wafungwa 100 katika Gereza hilo kwako katika mgomo wa kutokula, 21 kati yao wamekuwa wakilazimishwa kula kwa njia ya mipira ya puani.
 

Wataalam wa maswala ya haki za binaadam wamesema wamepokea taarifa juu ya madhara ya kisaikolojia na kimwili kufuatia kuwepo kwa sintofahamu juu ya mustakabali wa maisha yao.
 

Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia maswala ya haki za Binaadam mjini Geneva, Rupert Colville amesema kuwa Mamlaka nchini Marekani inakiuka Wajibu wao wa kulinda haki za binaadam kimataifa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.