Pata taarifa kuu
TUNISIA

Chama cha Ennahda nchini Tunisia chaachia Wizara muhimu nchini humo kwa Wanasiasa wasiogemea upande wowote

Chama cha kiislamu kinachotawala nchini Tunisia kimesema kuwa kimeridhia kuachia ngazi katika wizara mbalimbali nchini humo na kuwaachia watu wanasiasa wasioegemea upande wowote, hatua ambayo imeelezwa kuwa itatia chachu kuelekea uundwaji wa Serikali mpya na hatimae kumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo.

Kiongozi wa Chama tawala nchini Tunisia, Rached Ghannouchi
Kiongozi wa Chama tawala nchini Tunisia, Rached Ghannouchi REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Chama cha Ennahda, Rached Ghannouchi amethibitisha taarifa za kuachiwa wanasiasa hao Wizara nne ambazo ni Wizara ya mambo ya ndani, Sheria, Wizara ya mambo ya nje na Wizara ya ulinzi.
 

Ennahda imekua ikiongoza wizara ya mamabo ya ndani, Wizara ya Sheria na Wizara ya mambo ya nje tangu Tunisia ilipofanya uchaguzi wa kwanza ulio huru ambao ulifanyika Mwezi Oktoba mwaka 2011, miezi tisa baada ya kuangushwa kwa aliyekua Kiongozi wa Taifa hilo, Zine el Abidine Ben Ali.
 

Ghannouchi amesema kuwa Serikali mpya inaweza kuundwa mwishoni mwa Juma ambapo Serikali hiyo itavileta pamoja Vyama vya kiislamu na vile visivyo na mrengo wa kidini.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.