Pata taarifa kuu
ITALIA

Italia yashindwa kupata Mshindi wa uchaguzi wa wabunge

Uchaguzi wa wabunge nchini Italia umekumbwa na utata baada ya kubainika kuwa hakuna mshindi wa moja kwa moja.

Waziri Mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi
Waziri Mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi AFP PHOTO / OLIVIER MORIN
Matangazo ya kibiashara

Hii imebanika wazi baada ya karibu kura zote kuhesabiwa licha ya chama cha mrengo wa kushoto kushinda viti vya ubunge huku chama cha mrengo wa kulia kinachoongozwa na Waaziri Mkuu wa zamani Silvio Berlusconi wakisema wamepata viti vingi katika bunge la Senate.
 

Matokeo haya yanakuja wakati taifa hilo likikumbwa na hali ngumu ya kiuchumi.
Wanasiasa nchini humo wanasema kuwa wameshangazwa na matokeo hayo huku chama cha Waziri Mkuu wa zamani Berlusconi kikitaka wizara ya mambo ya ndani kutotangaza matokeo ya mwisho.
 

Chama cha mrengo wa kushoto kimepata asilimia 29 nukta 54 huku kile cha mrengo wa kulia kikipata asilimia 29 nukta 18.
 

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa huenda matokeo hayo yakabadilika ikiwa kura kutoka nje zitakapojumuishwa katika matokeo ya mwisho.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.