Pata taarifa kuu
DRC-ETHIOPIA

Viongozi wa Nchi za ICGLR washindwa kusaini makubaliano ya kupata amani ya kudumu Mashariki mwa DRC katika Mkutano wa Umoja wa Afrika AU

Makubaliano ya kusaini mkataba wa amani kusaka suluhu ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yaliyopangwa kufanyika jumatatu hii yameahirishwa kutokana na masuala kadhaa kushindwa kufikiwa muafaka. Maofisa wa Umoja wa Mataifa UN ambao wanahudhuria Mkutano wa Umoja wa Afrika AU ndiyo wamethibitsha hatua ya kushindikana kusainiwa kwa makubaliano baina ya serikali na Waasi wa M23 ambao wamekuwa vinara huko Mashariki mwa DRC.

Viongozi wa Nchi Wanachama za Umoja wa Afrika AU wakiwa Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia
Viongozi wa Nchi Wanachama za Umoja wa Afrika AU wakiwa Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN Ban Ki Moon, Eri Kaneko ndiye amethibitisha mataifa ambayo yamekuwa mstari wa mbelekatika kusaka suluhu ya Mashariki mwa DRC kukataa kusaini makubaliano hayo.

Kaneko ameshindwa kueleza kwa undani ni kwa nini mataifa hayo ambayo mengi yamekuwa mstari wa mbele kusaidia juhudi za kupatikana suluhu kukataa uamuzi wa kusaini makubaliano hayo huko nchini Ethiopia.

Mataifa yanayounda Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR ndiyo yalikuwa yanatarajiwa kusaini makubaliano hayo kutokana na hatua ambazo wamekuwa wakizitekeleza katika kuhakikisha DRC inapata amani ya kudumu.

Mataifa hayo ni pamoja na Tanzania, DRC, Afrika Kusini, Uganda, Rwanda, Angola, Burundi, Jamhuri ya Congo na Afrika Kusini lakini kuna kila dalili makubaliano hayo yamegongwa mwamba.

Tangazo la kusitishwa kwa kusaini kwa makubaliano lililotoewa dakika thelathini kabla ya kufanyika sherehe zilizoandaliwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika AU Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula amesema wamekataa kusaini makubaliano hayo kutokana Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC kwa kipindi chote kufanyakazi bila usaidizi wa Umoja wa Mataifa UN hivyo hawataki ushauri wao.

Waziri huyo wa Ulinzi amesema wanataka waendelea na juhudi zao wenyewe kwa sababu wametoka kugumu na sasa wanaelekea kupata suluhu ya mgogoro huo kutokana na Afrika Kusini, Tanzania na Angola kuwa tayari kupeleka wanajeshi Mashariki mwa DRC.

Hapo jana Rais wa Rwanda Paul Kagame na yule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ambao nchi zao zinatajwa kuwafadhili Waasi wa M23 walikataa kuzungumza chochote katika suala la kusainiwa kwa makubaliano hayo.

Umoja wa Mataifa UN kwa sasa kupitia Katibu Mkuu Ban unaangalia namna ya kuliingiza suala hilo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC ambapo atawasilisha mpango mpya wa kusaka amani ya kudumu.

Ban hiyo jana ametoa wito kwa Viongozi wa Ukanda wa Jumuiya ya Maziwa Makuu ICGLR kukubaliana na mpango wa amani na usalama kwa kushirikisha Taasisi nyingine ili kupata utulivu Mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.