Pata taarifa kuu
BRAZIL

Serikali ya Brazil yatangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kutokea kwa janga la moto lililouawa watu 231

Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo kutokana na janga la moto lililozuka kwenye Klabu moya ya Starehe ya Usiku iliyopo Kusini mwa Jiji la Santa Maria na kusababisha vifo vya watu mia mbili na thelathini na mmoja na wengine mamia wakiachwa na majeraha.

Kikosi cha Kuzima moto kikikabiliana na moto uliozuka kwenye Klabu ya Usiku na kuuawa watu 231
Kikosi cha Kuzima moto kikikabiliana na moto uliozuka kwenye Klabu ya Usiku na kuuawa watu 231
Matangazo ya kibiashara

Chanzo cha moto huo unatajwa ni Mwanamuziki mmoja kwenda kwenye jukwaa akiwa na mlipuko ambao ulishika katika eneo hilo na kuchangia kuzuka kwa moto mkubwa na watu kuanza kukanyagana kwa lengo la kunusuru maisha yao baada ya moto kuanza kusambaa kwa kasi.

Rais wa Brazil Dilma Roussef amelazimika kukatisha safari yake nchini Chile kuhudhuria Mkutano wa Kikanda na kulazimika kutembelea eneo ambalo limeathirika na moto huo ambao unaongeza hofu ya usalama wakati nchi hiyo ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia na Mashindano ya Olimpiki.

Moto huo umeteketeza sehemu kubwa sana ya Klabu hiyo ya Starehe ya usiku na Vikosi vya Kuzima moto vimeshuhudiwa vikikabiliana na moto huo usiku kucha lakini kwa kiasi kikubwa walionekana kuzidiwa kutokana na moto huo kuwa mkali na kuwa umeenea sehemu kubwa zaidi.

Jeshi la Polisi katika taarifa yake awali limesema kuwa sababu ya watu wengi kupoteza maisha baada ya kuzuka kwa moto huo ni kukosekana kwa hewa ya kutosha na kukanyagana wakati watu hao wakigombea kutoka nje huku Klabu hiyo ikikosa mlango wa dharura.

Wengi wa wale ambao wamepoteza maisha ni Wanafunzi wa Chuo Kimoja cha Sayansi katika Mji wa Santa Maria ambao walihudhuria kwa ajili ya kushuhudia tamasha hilo ambalo lilikuwa linajumuisha muziki wa moja kwa moja.

Wananchi wengi wameanza kuhoji hali ya usalama kabla ya Kombe la Dunia mwaka 2014 na Mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 ambayo yote yataandaliwa na Brazil wakiamini bado kuna klazi kubwa inapaswa kufanywa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.