Pata taarifa kuu
VENEZUELA-CUBA-BOLIVIA

Upinzani nchini Venezuela wataka kuwepo ukweli juu ya hali ya afya ya Rais Chavez

Chama Kikuu Cha upinzani nchini Venezuela kimeitaka serikali kueleza ukweli juu ya hali ya afya ya Rais Hugo Chavez ambaye anaendelea kupatiwa matibabu nchini Cuba kutokana na uwepo wa uvumi hali yake ni tete.

Rais wa Venezuela Hugo Chavez ambaye anaendelea kupatiwa matibabu ya saratani nchini Cuba
Rais wa Venezuela Hugo Chavez ambaye anaendelea kupatiwa matibabu ya saratani nchini Cuba
Matangazo ya kibiashara

Upinzani nchini Venezuela umeshusha lawama kwa serikali kwa kile ambacho wanakitaja imeshindwa kuweka bayana ukweli wa mambo juu ya afya ya Kiongozi wa Taifa hilo ambaye licha ya kusumbuliwa na saratani ana magonjwa mengine nyemelezi.

Kiongozi wa Muungano wa Vyama Vya Upinzani chini ya Mwamvuli wa MUD nchini Venezuela Ramon Guillermo Aveledo amesema ni vyema serikali ikawa na uhakika na inachokisema na kuwaeleza ukweli wananchi wake.

Aveledo ameitaka serikali kuacha kuficha chochote kinachohusiana na afya ya rais Chavez kutokana na wananchi kuhitaji kufahamu kila hatua ya matibabu ya Kiongozi huyo anayetarajiwa kuapishwa baadaye mwezi huu.

Kauli hii inakuja huku mkwe wa Rais Chavez, Jorge Arreaza akituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa tweeter akisema Kiongozi huyo ameshapona japokuwa afya yake bado haijatengamaa ipasavyo.

Haya yanakuja kipindi hiki ambacho Rais wa Bolivia na rafiki mkubwa wa Chavez, Evo Morales akisema ana matumaini makubwa sala ambazo wamezifanywa zitasaidia kumponesha Kiongozi huyo mwenye msimamo.

Ombi la Upinzani linakuja siku moja baada ya Makamu wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro kutangazia umma hali ya afya ya Kiongozi wao imeanza kuimarisha baada ya kufanyiwa upasuaji majuma matatu yaliyopita.

Maduro aliwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi wa aina yoyote kutokana na yeye mwenyewe kuzungumza na Rais Chavez mara mbili katika kipindi cha siku yayu hatua ambayo imethibitisha ameanza kupona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.