Pata taarifa kuu
Italia

Shirika la Chakula duniani, FAO laripoti wimbi la Nzige eneo la Kaskazini Magharibi mwa Afrika

Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa wimbi la Nzige huenda likaelekea kaskazini Magharibi mwa Afrika Majuma ya hivi karibuni ,na kutoa wito wa kunyunyizwa dawa kwenye Mazao ili kuyakinga mazao hayo dhidi ya Nzige.

Nzige wamekuwa wakiripotiwa na shirika la Chakula duniani, FAO kuwa ni  Hatari katika Maeneo ya kaskazini Magharibi mwa Afrika
Nzige wamekuwa wakiripotiwa na shirika la Chakula duniani, FAO kuwa ni Hatari katika Maeneo ya kaskazini Magharibi mwa Afrika
Matangazo ya kibiashara

Algeria, Libya, Mauritania na Morocco zimetaadharishwa kuwa tayari na kuhakikisha kuwa wanafanya jitihada za kupambana na Nzige, taarifa ya shirika la Chakula duniani, FAO limeeleza.
 

Imeelezwa kuwa kundi dogo la Nzige hula chakula kinachoweza kuliwa na Watu 35,000 kwa siku.
 

Kundi hilo la nzige wanazaliana nchini Chad na kuwa wanatarajiwa Mali na Niger pia kufuatia Mvua za kukuzia ambazo zinasababisha ongezeko la Nzige.
 

Shirika la FAO limesema kuwa limekuwa likifuatilia kwa karibu hali ilivyi nchini Niger na Chad lakini wamekuwa wakipata ugumu nchini Mali kufuatia Machafuko ya nchini humo.
 

Shirika hilo limesema Operesheni za kumwagilia dawa zilianza nchini Chad mwanzo ni mwa Mwezi Oktoba na kuwa Operesheni hiyo inaelekea kuanza, nchini Niger, hata hivyo Timu hizo zitaambatana na Msafara wa Wanajeshi kwa ajili ya Usalama.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.