Pata taarifa kuu
DRCONGO-FRANCOPHONIE

Waziri wa Ufaransa wa Francophonie azuru mashariki mwa DRCongo wakati mkutano ukikomeshwa jijini Kinshasa

Waziri wa Ufaransa anaehusika na maswala ya Francophonie Yamina Benguigui anazuru mji mkuu wa Mkoa wa kivu ya Kaskazini wa Goma, mashariki mwa jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC eneo linalo kabiliwa na machafuko ya mapigano baina ya majeshi ya serikali na vikosi vya waasi wa M23.

Viongozi wa jumuiya ya nchi zinazo zungumza lugha ya kifaransa Octoba 13,  2012 jijini Kinshasa.
Viongozi wa jumuiya ya nchi zinazo zungumza lugha ya kifaransa Octoba 13, 2012 jijini Kinshasa. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Yamine Benguingui anatarajia kutia sahihi kwenye makubaliano ya kutowa msaada kwa wakimbizi walioyatoroka ma kwako kutokana na machafuko katika eneo hilo.

Wakati hayo yanajiri, viongozi wa Jumuiya ya nchi zinazo zungumza lugha ya kifaransa Francophonie, wameomba vikwazo vichukuliwe zaidi kwa watu wanaohusika na machafuko mashariki mwa DRCongo wakati wakihitimisha jana jumapili jijini Kinshasa mkutano wa kilele wa Jumuiya hiyo, uliomalizika huku serikali ya Kinshasa ikikanusha tuhuma za kutoupa nafasi upinzani, hivyo kuipokonya demokrasia.

Rais Joseph Kabila alitumia fursa ya mkutano wa mwisho na vyombo vya habari na kuzungumzi kuhusu mambo mbalimbali yaliotuama mazumgumzo yake na viongozi mbalimbali akiwemo Francois Hollande ambae aliwasili jijini Kinshasa Jumamosi na kuondoka siku hiyo hiyo jioni.

Rais Kabila amesema kwamba RDCongo inapendezwa na demokrasia iliopo nchini humo na kuongeza kuwa jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo haina aibu yoyote kuhusu kiwango cha demokrasia na haki za bindamu, Uhuru, na hali ya haki za binadamu. Amesisitiza kuwa wanatumia mfumo wa demokrasia nchini humo kwa imani na wala sio kwa shinikizo.

Awali rais wa Ufaransa Francois Hollande alitamka kuwa hali ya haki za binadamu, demokrasia na haki za wapinzani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo havikubaliki.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.