Pata taarifa kuu
MAREKANI

Mdahalo wa wagombea wenza makamu wa rais watikisa Marekani

Wagombea wa nafasi ya makamu wa rais kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani Joe Biden wa Chama cha Democrats na Paul Ryan kutoka chama cha Republican usiku wa kuamkia leo kwa saa za hapa Afrika Mashariki wamechuana vikali kwenye mdahalo wao wa kwanza wa Kihistoria huku suala la Iran na Syria likitawala mjadala wao.

REUTERS/Michael Reynolds
Matangazo ya kibiashara

Mdahalo huo ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu kuona namna ambavyo wagombea hao watanadi sera za wagombea wa urais waliochuana juma moja lililopita, umeshuhudia wagombea wote wawili wakirushiana maneno makali kuhusu sera ya mambo ya nje ya Marekani.

Mjadala kuhusu suala la Iran ndio ulioibua hisia kali toka kwa wagombea wote wawili huku, Paul Ryan wa chama cha republican akiendelea kuikosoa serikali ya Rais Barack Obama akidai imeshindwa kutenda kuhusu kuidhibiti nchi ya Iran na utengenezaji wa silaha za maangamizi.

Kauli hiyo ilipingwa vikali na Mgombea wa Democrats Joe Biden ambaye mara zote alionekana kujiamini kwakuwa na uzoefu wa muda mrefu kwenye bunge la Congress ambapo hakusita kumkosoa mpinzani wake akihoji wao watafanya nini kuhusu Iran wakati wanataka kutumia nguvu kutatua mgogoro wa masharki ya kati.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanaona kuwa makamu wa rais Joe Biden kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kuziba mapunguzfu yaliyoonyeshwa na rais baeack Obama kwenye mjadala kati yake na Mitty Romney na kumfunika kabisa kijana Paul Ryan.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.