Pata taarifa kuu
MAREKANI

Obama aendelea na kampeni, mdahalo wa wagombea wenza kufanyika leo

Rais wa Marekani Barack Obama ambaye anawania kutetea kiti chake kupitia chama cha Demokrats ameendelea na kampeni zake huku akisisitiza kutofanya makosa kama aliyoyafanya kwenye mdahalo wa kwanza dhidi ya mpinzani wake Mitty Romney.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mdahalo wa awali Obama alionekana kuwa mpole zaidi kwa Mitty Romney hali iliyomfanya mgombea huyo wa chama cha Republican kujiongezea umaarufu kwenye kampeni zake.

Lakini wakati Obama na Romney akisubiri kurejea kwenye mdahalo wa awamu ya pili hii leo usiku wagombea wenza kwenye nafasi ya makamu wa rais Joe Biden wa chama cha Democrats na Paul Ryan toka republican.

Wagombea hao wanatarajiwa kuchuana kwenye mdahalo mwingine amabo unasubiriwa kwa hamu kuwa na maelfu ya wananchi wa Marekani.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanampa nafasi kubwa Joe Biden kung'ara kwenye mdahalo huo licha ya Ryan nae kupewa nafasi.

Wakati huohuo Jumuiya ya kimataifa imeendelea kulaani shambulio ambalo limefanywa na wapiganaji wa Taliban nchini Pakistan dhidi ya msichana Malala Yousef ambaye alikuwa akipigania haki za watoto nchini humo kupata elimu.

Rais wa Marekani Barackm Obama na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon wameeleza kusikitishwa na shambulio hilo na kuliita ni lakikatili dhidi ya mtoto asiye na hatia.
Hapo jana maelfu ya wananchi wameandamana nchini humo kupinga shambulio hilo la Taliban huku serikali ikitangaza donge nono kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa watu waliotekeleza shambulio hilo.

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.