Pata taarifa kuu
MAREKANI

Baraza la usalama la umoja wa mataifa la laani vikali mashambulizi katika balozi za Marekani.

Baraza la Usalama la umoja wa mataifa limelaani vikali mashambulizi ya jana Ijumaa yaliyotekelezwa katika balozi za Marekani, wakati vurugu zikiendelea kushika kasi dhidi ya filamu ya Marekani inayodaiwa kumdhihaki Mtume Mohammed. 

portugal-india.com
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa Baraza la Usalama wameonesha hisia zao za ndani kufuatia mashambulizi hayo na kukumbusha kuwa balozi zipo kwa malengo ya kidiplomasia na amani na kwamba miongoni mwa majukumu muhimu ya mabalozi ni kukuza maelewano bora katika nchi na tamaduni mbalimbali.

Akisoma taarifa ya baraza hilo Balozi wa ujerumani Peter Wittig ambaye ndiye rais wa sasa wa baraza hilo,ametoa ukumbusho wa kanuni ya msingi ya kukiuka haki za majengo ya balozi na kusema kuwa mashambulizi hayo hayakubaliki.

Ghasia mpya zilizuka huko Yemen na Cairo na maandamano yakafanyika katika mataifa ya Bangladesh, Indonesia, Malaysia, Pakistan, Iraq, Israel na Ukanda wa Gaza, Morocco, Syria, Kuwait, Nigeria na Kenya, baada ya balozi wa Marekani nchini Libya na wafanyakazi wenzake watatu kuuawa katika ubalozi wa Marekani katika mji wa mashariki wa Benghazi.

Wakati huo huo
Rais wa Marekani Barack Obama ameapa kusimama imara dhidi ya kuenea kwa mapambano makali dhidi ya taifa hilo katika mataifa ya Kiarabu, wakati akiomboleza vifo vya wamarekani wanne waliouwawa nchini Libya baada ya mabaki yao kufikishwa nchini humo.

Aidha rais Obama amelihakikishia taifa hilo kuwatia hatiani waliohusika na mauaji ya balozi Chris Stevens na watumishi wenzake watatu.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.