Pata taarifa kuu
Marekani

Rais Obama apongeza umoja wa Marekani

Rais wa Marekani Barack Obama amepongeza umoja ambao wameuonesha wananchi wa taifa hilo katika kipindi ambacho wamefanya kumbukizi ya miaka kumi na moja tangu kutokea kwa mashambulizi ya tarehe kumi na moja mwezi September.

Barack Obama
Barack Obama REUTERS/Jim Young
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo la kigaidi ambalo lilitekelezwa nchini Marekani lilisabbaisha vifo vya watu zaidi ya elfu tatu na kuangusha majengo mawili ambayo yalikuwa yanatumiwa kwa masuala ya biashara.

Mtandao wa Al Qaeda ndiyo ambao ulipanga na kisha kutekeleza shambulizi hilo ambalo liliacha maelfu ya watu wakijeruhiwa na hapa Rais Obama anaeleza hali ilivyo kwa sasa baada ya tukio hilo baya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.