Pata taarifa kuu
MEXICO

Enrique Pena Nieto atangazwa rais mteule wa Mexico

Rais mteule wa Mexico Enrique Pena Nieto, ametoa wito kwa taifa hilo kuungana mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa rais mteule baada ya miezi miwili ya ucheleweshwaji wa kisheria kuhusu mzozo baina yake na mpinzani wake ambaye hata hivyo amekataa kukiri kushindwa. 

blogs.cfr.org
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho ya mahakama ya uchaguzi nchini humo imemtangaza rasmi Pena Nieto kuwa mshindi wa uchaguzi wa Julai 1 baada ya kutupilia mbali jaribio la kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto kupinga matokeo kwa madai kuwa Nieto alinunua kura.

Maamuzi hayo yanasafisha njia kwa Pena Nieto kuanza muhula wake wa miaka sita Desemba mosi, na kuashiria kurudi madarakani kwa chama cha Institutional Revolutionary Party PRI baada ya kukosekana kwa miaka 12.

Rais anayemaliza muda wake Filipe Calderon atawasilisha hotuba yake ya mwisho taifa hilo kwa njia ya maandishi kwenye bunge jipya.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.