Pata taarifa kuu
Uingereza

Julian Assange ataka Marekani isitafute mchawi wa matatizo yake

Mmiliki wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange ameishutumu vikali serikali ya Uingereza na Marekani na kuzitaka nchi hizo kuacha kutafuta mchawi wa matatizo yao kupitia mtandao wake.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Assange ambaye amejitokeza siku ya Jumapili kwa mara ya kwanza toka aombe hifadhi kwenye ubalozi wa Ecuador alishangiliwa na maelfu ya wananchi waliojitokeza nje ya Ubalozi huo.

Assange alitoa shukrani zake kwa serikali ya Ecuador na raia wa nchi za kusini mwa bara la America kwa kumuunga mkono.

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi za kusini mwa bara la Amerika jana walitoa taarifa yao na kuyashutumu mataifa ya Uingereza na Marekani kutaka kuingilia uhuru wa vyombo vya habari na kutishia maisha ya watu.

Wakati huohuo Serikali ya New Zealand hii leo imetangaza kuwa itahakikisha vikosi vyake vilivyoko nchini Afghanistan vinaondoka nchini humo mapema zaidi kufuatia hapo jana kuuawa kwa askari wake watatu.

Waziri mkuu wa New Zealand John Key, amesema kuwa mtu mmoja alijitoa muhanga kwenye gari la wanajeshi wa nchi hiyo na kuua askari wake watatu waliokuwa kwenye doria.

Licha ya shambulio hilo nchi hiyo imesema haitasitisha misaada mingine kwa nchi ya Afghanistan badala yake itaendelea kutoa msaada utakaohitajika na Serikali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.