Pata taarifa kuu
AFGANISTAN

Wanajeshi 11 wa NATO wafariki kutokana na ajali ya ndege nchini Afganistan

Ndege ya kijeshi ya NATO ikiwa na wanajeshi wa kimataifa imeanguka Kusini mwa Afganistan na kusababisha vifo vya wanajeshi 11.

Matangazo ya kibiashara

NATO inasema wanajeshi waliuawa kutokana na mkasa huo uliotokea Alhamisi asubuhi ni wanajeshi saba wa Marekani na wanne wa Afganistan.

Kundi la kigaidi la Taliban linadai kuidungua nege hiyo ya NATO kwa mujibu wa msemaji wake Qari Yusuf Ahmadi.

Hata hivyo, NATO imesema inachunguza kiini cha ajali hiyo kabla ya kutoa ripoti yake kamili kueleza ni vipi mkasa huo ulitokea.

Mwezi wa Agosti mwaka uliopita,Taliban iliiangusha ndege nyingine ya kijeshi ya NATO karibu na mji wa Kabul na kusababisha kuuawa kwa wanajeshi 30 wa Marekani na wengine nane wa Afganistan.

Majeshi ya NATO yanatarajiwa kuondoka nchini Afganistan ifikapo mwisho wa mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.