Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Vikosi vya NATO hatimaye vyaingiza vifaa vyao katika Mpaka wwa Pakistan baada ya kufungwa kwa Miezi Saba

Vifaa vya Majeshi ya kujihami ya nchi za Magharini, NATO vimeingia katika Mpaka wa Pakistan kwa mara ya pili tangu Islamabad ilipofungua Mipaka yake baada ya kuifunga kwa kipindi cha Miezi saba. 

Vikosi vya NATO vikiwa katika Operesheni dhidi ya Taliban
Vikosi vya NATO vikiwa katika Operesheni dhidi ya Taliban Reuters
Matangazo ya kibiashara

Pakistan ilifunga njia na kufanya Msafara wa NATO kutoingia nchini humo baada ya tukio la Shambulio la Anga lililotekelezwa na Majeshi ya Marekani na kusababisha Wanajeshi 24 kupoteza maisha mwezi Novemba na kuteteresha mahusiano kati ya Marekani na Pakistan.
 

Islamad imefikia hatua hiyo baada ya Waziri wa Mambo ya wa Marekani, Hillary Clinton alipoomba radhi kwa tukio hilo.
 

Mpaka hii leo Magari machache yameruhusiwa kuingia Afghanistan huku maelfu ya Wamiliki wa Magari wakisubiri kulipwa fidia kabla ya kurudi tena kazini wakisema kuwa Safari za nchini Afghanistan ni za hatari na Malipo hayakidhi.
 

Kundi la Wanamgambo wa Taliba wametishia kushambulia Magari ya NATO na kuwaua Madereva ikiwa wataanza tena Safari nchini Afghanistan.
 

Hii leo Wapiganaji hao wametishia kufanya Mashambulizi na kudai wao ndio waliohusika na shambulizi la kuwafyatulia Risasi Maafisa Polisi tisa wanaopata Mafunzo Mashariki mwa Mji wa Lahore.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.