Pata taarifa kuu
ARGENTINA

Watawala wa zamani wa Kijeshi nchini Argentina wahukumuwa kifungo kwa kosa la Utekajinyara watoto

Mahakama nchini Argentina imetoa adhabu kali kwa Madikteta wawili nchini humo ambalo walihudumu wakati nchi hiyo inatawaliwa na Jeshi katika kipindi cha mwaka elfu moja mia tisa sabini na sita hadi mwaka elfu moja mia tisa themanini na tatu. Madikteta hao wawili ni Jorge Videla mwenye umri wa miaka 86 ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka hamisni jela na mwenzake Reynaldo Bognone mwenye umri wa miaka 84 aliyehukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano jela.

Viongozi wa zamani wa Kijeshi nchini Argentina Reynaldo Bignone na Jorge Videla ambao wamehukumiwa kifungo kwa kosa la utekejinyara watoto
Viongozi wa zamani wa Kijeshi nchini Argentina Reynaldo Bignone na Jorge Videla ambao wamehukumiwa kifungo kwa kosa la utekejinyara watoto
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Majaji Maria Roqueta ndani ya chumba cha Mahakama Kuu huko Buenos Aires ndiye aliyetangaza hukumu dhidi ya madikteta hao wawili baada ya kuwakuta na hatia ya kuteka nyara watoto wadogo.

Hukumu hiyo inakuja wakati ambapo madikteta hayo wawili Videla na Bignone wakiwa wameshahukumiwa kifungo kutokana na kutenda makosa ya uhalifu wa kivita wakati wa utawala wa kijeshi nchini humo.

Watoto wanaokadiriwa kufikia mia nne walitekwa kisha kutenganishwa na familia zao na Madikteta hao ambao walikuwa walishirikiana na watu wengine katika kufanikisha mpango wao huo.

Mamia ya wananchi wakiwemo ndugu wa waathirika, watoto waliungana na familia zao na wanaharakati wamefurahishwa sana na hukumu hiyo na kusema kwa namna moja ama nyingine haki imetendeka.

Maofisa wengine wa zamani wa Kijeshi tayari wameshahukumiwa kifungo cha kufikia hadi miaka arobaini jela kutokana na kuhusika kwenye kupanga mpango wa kuwateka nyara watoto.

Washtakiwa wawili kati ya kumi na moja ambao walikuwa wanahusishwa na mpango huo wa utekeji nyara watoto waliachiwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kuwatia hatiani kama wamehusika kwenye mpango huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.