Pata taarifa kuu
LOC CABOS-MEXICO

Nchi wanachama za G20 waitaka dunia kukabiliana na changamoto za kiuchumi

Mkutano wa nchi za G20 uliokuwa unafanyika kwenye mji wa Los Cabos nchini Mexico umemalizika huku nchi wanachama zikikubaliana kuongeza funguzi la fedha zaidi kwa shirika la fedha duniani IMF kusaidia kukopesha nchi zilizoko kwenye mtikisiko wa uchumi.

Rais wa Mexico Felipe Calderon ambaye nchi yake ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa G20
Rais wa Mexico Felipe Calderon ambaye nchi yake ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa G20 REUTERS/Mariana Bazo
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mkutano wao, rais wa Mexico ambaye ndie mwenyejei wa mkutano huo Felipe Calderon amesema kuwa ni lazima mataifa yaungane katika kuhakikisha zinakabiliana na changamoto za kiuchumi.

Wakati wakihitimisha mkutano wao viongozi hao kwa kauli moja wamekubaliana kuongeza mara mbili zaidi ya fedha za awali ambazo shirika la fedha duniani IMF ilikuwa imeomba ambapo sasa zitachangia dola za Marekani bilioni 456.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani IMF, Christine Lagarde amepongeza hatua ambayo imefikiwa na nchi wanachama za G20 na kusema kuwa fedha hizo sasa zitasaidia kuzikopesha nchi za Ulaya ambazo zimeendelea kuwa kwenye mdororo wa kiuchumi.

Lagarde ameongeza kuwa tayari wamekwisha wasiliana na serikali ya Ugiriki katika kufufa mazungumzo mapya kuhusu kupatiwa mkopo wa dola bilioni 130 kama mkopo kwaajili ya kusaidia kuinua uchumi wa mataifa hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.