Pata taarifa kuu
UINGEREZA-SWEDEN-AUSTRALIA

Mahakama Kuu Nchini Uingereza yatupilia mbali rufaa ya Julia Assange kupingwa kupelekwa Sweden

Mwazilishi na Mmiliki wa Mtandao wa Habari za Kichunguzi Duniani wa WikiLeaks Julian Assange ameshindwa kwenye rufaa yake aliyokuwa anapinga kupelekwa nchini Sweden kukabiliana na mashtaka ya ubakaji anayotuhumiwa kuyatenda.

Mwanzilishi na Mmiliki wa Mtandao wa Kichunguzi wa WikiLeaks Julian Assange ambaye rufaa yake imetupiliwa mbali na Mahakama Kuu Nchini Uingereza
Mwanzilishi na Mmiliki wa Mtandao wa Kichunguzi wa WikiLeaks Julian Assange ambaye rufaa yake imetupiliwa mbali na Mahakama Kuu Nchini Uingereza REUTERS/Stefan Wermuth
Matangazo ya kibiashara

Assange ameshindwa kwenye rufaa hiyo ambayo aliikata katika Mahakama Kuu Nchini Uingereza akitaka kesi hiyo isikilizwe katika nchi nyingine na Sweden kama ambavyo mahakama za nchi hiyo zinavyotaka.

Majaji wa Mahakama Kuu nchini Uingereza ambao walikuwa wanasikiliza rufaa hiyo iliyowasilishwa na Assange wamekubaliana na hati iliyowasilishwa na Mwendesha Mashtaka wa Sweden akitaka Mmiliki huyo wa WikiLeaks arejeshwe nyumbani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Jopo la Majaji saba ndiyo ambao walikuwa wanasikiliza pingamizi la Assange ambapo watano walilutipilia mbali na wengine wawili waliunga mkono hatua ya Mmiliki huyo wa WikiLeaks kupinga kuhukumiwa nchini Sweden.

Hukumu hiyo ina maana Assange sasa atapelekwa nchini Sweden kukabiliana na mashtaka yake lakini tayari Mwanasheria wake amesema atakata rufaa tena kupinga uamuzi huo wa kumpeleka mteja wake kukabiliana na mashtaka ya ubakaji.

Hii ina maana Assange ataendelea kuwepo nchini Uingereza kwa siku kumi na nne pekee kabla ya kupelekwa Sweden na wakati hukumu hiyo inatolewa yeye hakuwepo Mahakamani na badala yake aliwakilishwa na mwanasheria wake.

Assange ambaye ni raia wa Australia alikamatwa nchini Uingereza mwezi Desemba mwaka 2010 baada ya mtandao wake wa WikiLeaks kuchapisha taarifa za siri za nchi ya Marekani na mataifa mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.