Pata taarifa kuu
MEXICO

Polisi nchini Mexico wabaini miili ya watu 15 waliouawa na kutelekezwa kwenye gari kaskazini mwa nchi hiyo

Polisi nchini Mexico imefanikiwa kubaini miili ya watu 18 waliokatwa vichwa katika magari mawili yaliyotelekezwa magharibi mwa nchi hiyo, tukio ambalo linahusishwa na mauaji ya kulipiza kisasi ya makundi ya uuzaji wa dawa za kulevya.

Maofisa usalama nchini Mexico wakiondoa miili ya watu waliokutwa wameuawa kaskazini mwa nchi hiyo
Maofisa usalama nchini Mexico wakiondoa miili ya watu waliokutwa wameuawa kaskazini mwa nchi hiyo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Polisi mji wa Jalisco ambako ndiko miili hiyo imepatikana amethibitisha kupatikana kwa miili ya watu hao 18 ambao amesema wameuawa kikatili kwa kukatwa shingo na kuongeza kuwa wanaendelea na uchunguzi kubaini kiini cha kufanyika kwa mauaji hayo.

Mwanasheria wa jimbo la Jalisco Tomas Coronado Olmos ameitisha mkutano wa dharura akisema kuwa mauaji hayo yamelipa kisasi cha mauaji ya watu 23 yaliyotokea ijumaa ya juma lililopita kaskazini mashariki mwa mji wa Tamaulipas.

Mamlaka nchini Mexico imeshutumu magenge mawili ya Zetas na lile la Sinaloa Federation of Mexico, ambalo mkuu wa kundi hilo Joaquin Guzman amekuwa akisakwa na mamlaka ya nchi hiyo.

Zaidi ya watu hamsini elfu wameuwa wakihusishwa na ugomvi wa biashara ya dawa za kulevya huku Rais wa nchi hiyo akitangaza vita kati ya vikosi vyake na magenge ya wafanyabiashara hao

Rais wa nchi hiyo Felipe Caledrone ametangaza vita dhidi ya makundi yanayojihusisha na biashara haramu ya uuzaji wa dawa za kulevya ambayo yamekuwa yakitekeleza mauaji kwenye kumbi za starehe pamoja na maofisa wa polisi ambao wamekuwa mstari wa mbele kupambana na makundi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.