Pata taarifa kuu
MAREKANI

Kinara wa mashambulizi ya Septemba 11 kujibu mashitaka, Marekani kupeleka balozi Myanmar

Marekani hatimaye imetangaza utayari wake wa kumfikisha kwenye mkono wa sheria kinara wa mashambulizi ya tarehe kumi na moja mwezi Septemba nchini humo Khalid Sheikh Mohammed pamoja na wenzakr wanne ambao wanshikiliwa kwenye gereza la Guantanamo.

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama REUTERS/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Marekani unakuja kutokana na kile ambacho wanasema huu ni wakati muafaka kwa mtuhumiwa huyo na wenzake kuweza kufikishwa Mahakamani na kujibu mashtaka ambayo yanamkabili ya ugaidi.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jay Carney amethibitisha utayari wa kufikishwa katika Mahakama ya Kijeshi kwa Khalidi na wenzake wanne huku akiendelea kusisitiza nia ya Rais Barack Obama ni kufunga Gereza la Guantanamo.

Marekani imetangaza utayari wa kuondoa vikwazo kwa nchi ya Myanmar na kuhakikisha wanaisaidia kufanya mabadiliko ya kidemokrasia sambamba na kurejesha maridhaino ya kitaifa katika nchi hiyo iliyopitia kwenye Utawala wa Kidikteta.

Uamuzi wa Marekani umekuja siku kadhaa baada ya Kiongozi Upinzani nchini Myanmar na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Aung San Suu Kyi kushindi kwenye uchaguzi mkdogo wa ubunge nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ndiye ambaye ametoa kauli ya utarai wa nchi yake kutekeleza hayo yote huku akisema ni lazima wananchi wa Myanmar wapate maendeleo yatakayochangiwa na utawala bora.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.