Pata taarifa kuu
IRAQ-UMOJA WA NCHI ZA KIARABU

Viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu wakubaliana kwa kauli moja kuhusu mpango wa Annan

Mawaziri wa nchi za nje wa Jumuia ya nchi za Kiarabu waliokutana jana jijini Baghdad, wamekubaliana kuhusu mpango wa azimia kuhusu Syria unaotowa wito kuhusu rasimu ya  Umoja wa Mataifa iliopendekzwa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa UN Kofi Annan, ambae kwa sasa ni mjumbe wa UN na Jumuiya ya nchi za Kiarabu nchini Syria.

Kikao cha viongozi wa Jumuiya ya nchi za kiarabu katika kikao chao jijini Baghdad
Kikao cha viongozi wa Jumuiya ya nchi za kiarabu katika kikao chao jijini Baghdad
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwenye mkutano huo wa kilele wa Jumuiya ya nchi za kairabu, Hoshyar Zebari, waziri wa mambo ya nje wa Iraq, amesema "mgogoro wa Syria hauhusu pekee taifa mmoja la Kiarabu, bali unaathiri jumuiya nzima ya kimataifa", na ametowa wito wa kuwa na "mtazamo wa pamoja" wakati inapohitajika kutatua masuala ya kikanda.

Siku ya Jumanne Kofi Annan mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu alitangaza kwamba rais Bashar Al Assad alikubali mapendekezo ya amani yenye vifungo sita yatayopelekea kusitishwa kwa ghasia nchini humo.

Mapendekezo ya Kofi Annan yanaagiza kuondoa kwa silaha nzitonzito na askari kutoka kwenye vituo vyenye idadi kubwa ya watu, kuruhusu misaada ya kibinadamu, kufunguliwa kwa wafungwa kuruhusu mienendo ya nenda rudi na upatikanaji kwa waandishi wa habari. Pia inatoa wito wa kusitisha mapigano kwa muda ili kuruhusu misaada ya kitabibu na kibinadamu.

Mataifa ya Kiarabu yalirejesha nyuma mapendekezo yao ya awali, ambayo yalitaka kuondolewa kwa utawala Assad, baada ya Urusi na China kutumia kura ya turufu mara mbili mfululizo kupinga maazimio ua rasimuya Umoja wa Mataifa kulaani serikali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.