Pata taarifa kuu
MEXICO

Papa Benedict XVI Ziarani nchini Mexico aiasa jamii kuwalinda watoto

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa benedict wa 16 ambae anatembelea nchini Mexico, ametoa wito kwa jamii kuwajali na kuwalinda watoto sambamba na kutuma ujumbe maalumu kwa kundi lililoathirika baada ya ghasia.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani,Papa Benedict xvi
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani,Papa Benedict xvi Reuters/Alessia Pierdomenico
Matangazo ya kibiashara

Huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia papa Benedict wa 16 alitaja kashfa ya matendo mabaya dhidi ya watoto inayomuhusisha kuhani wa katoliki katika kipindi cha hivi karibuni.

Hii ni ziara ya pili kwa kiongozi huyo kutembelea bara lenye idadi kubwa ya wakatoliki duniani akisisitiza kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya na vitendo viovu dhidi ya ubinadamu.

Katika ziara yake kiongozi huyo wa katoliki duniani anatarajia kujadili mambo mbalimbali na raisi Felipe Caldero ikiwemo masuala ya uhalifu uliokithiri pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.