Pata taarifa kuu
Ufaransa

Maswali yaulizwa kuhusu uwezo wa Ufaransa kukabiliana na Ugaidi, waliouawa wakumbukwa

Maswali yameanza kuulizwa ni vipi mshukiwa wa kigaidi Mohamed Merah alivyotekeleza mauji ya watu saba Kusini mwa Ufaransa,wakiwemo watoto watatu katika shule ya Kiyahudi mjini Toulouse.

Matangazo ya kibiashara

Aidha,uwezo wa maafisa wa Inteljensia nchini Ufaransa unatiwa shaka kwa kutofaulu  kumkamata mshukiwa huyo mapema  licha ya kuwa katika orodha ya magaidi waliokuwa wanatafutwa nchini Ufaransa.

Mamia ya watu walikusanyika katika mji wa Toulouse kuwakumbuka watu saba waliouawa kwa kupigwa risasi na mshukiwa huyo.

Waziri Mkuu wa Francois Fillon amekosoa wale wanaoilaumu idara ya ujasusi kwa kushindwa kumkamata Merah mapema kwa kile alichokieleza kuwa,maafisa wa usalama  hawakuwa na sababu zozote za kumkamata mshukiwa huyo kabla ya kutekeleza mauji hayo.

Rais Nicolas Sarkzoy ambaye alirejelea kampeni zake za uchaguzi wa urais siku ya Alhamisi alisema mashambulizi hayo hayakupangwa na mwenda wazimu bali yalipangwa na  gaidi.

Sarkozy aliongeza kuwa serikali yake inafanya msako mkubwa kuwatafuta magaidi wanaoshi au kutekeleza majukumu yake nchini Ufaransa kwa njia ya mitandao na pia wanaosafiri katika nchi za kigeni wakitokea nchini Ufaransa.

Mohammed Merah aliuliwa kwa kupigwa risasi kichwani wakati alipokuwa anaruka kutoka dirishani siku ya Alhamsi katika makabiliano na polisi katika makaazi yake baada ya kukataa kujisalimisha katika juhudi zilizofanywa kwa zaidi ya saa 30 na polisi wa Ufaransa.

Kabla ya kuuwa  kwake mshukiwa huyo,alikiri kutekeleza mauji hayo na pia kuwa mwanamgambo wa Al-Qaeda aliyepata mafunzo kutoka Pakistan na Afganistan.

Kwa mujibu wa kiongozi wa mashtaka nchini Ufaransa Francois Molins, Merah alichukua video ya namna alivyotekeleza mauji hayo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.