Pata taarifa kuu
Ufaransa

Polisi Kusini mwa Ufaransa kwa siku ya pili wamzingira mshukiwa wa mauji,waendelea kumshawishi ajisalimishe

Polisi mjini Toulouse Kusini mwa Ufaransa kwa siku ya pili wanamzingira mshukiwa wa mauji ya watu wanne katika shule ya Kiyahudi siku ya Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Mohammed Merah raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria mwenye umri wa miaka 23,anatuhumiwa pia kutekeleza mauji ya wanajeshi watatu wa Ufaransa wiki mbili zilizopita.

Milipuko ya risasi imesikika usiku kucha katika oparesheni hiyo katika makaazi ya mshukiwa huyo na polisi wanasema wanaendelea kuzungumza naye kumtaka ajisalimishe ili wamkamate na kumfungulia mashtaka.

Mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya kupambana na ugaidi Francois Molins amesema Merah hajutii kitendo alichokifanya ingawa hakupata muda wa kutosha kuua watu wengine zaidi.

Molins ameongeza kuwa Merah amekiri kuhusika na mauaji hayo akidai alikuwa akilipiza kisasi kuhusu vifo vya raia wa Palestina na kupinga kuhusika kwa jeshi la Ufaransa kuhusika katika Operesheni zake nchini Afghanistan na hatua ya Ufaransa ya kupiga marufuku kwa wanawake kufunika nyuso zao kwa ushungi.

Watoto hao waliouawa walizikwa jana mjini Jerusalem nchini Israel katika mazishi yaliyohudhuriwa na maelfu ya waombolezaji pamoja waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Allain Juppe.

Rais Nicolas Sarkozy amesema mauji hayo hayataligawa taifa la Ufaransa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.