Pata taarifa kuu
Ufaransa

Rais Sarkozy aongoza kimya cha dakika moja kuwakumbuka watu wanne waliopigwa risasi Kusini mwa Ufaransa

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkzoy amesitisha kampeni zake za kisiasa na kuongoza kimya cha dakika moja kuwakumbuka watoto watatu  pamoja na mwalimu wao waliouawa siku ya Jumatatu kwa kupigwa risasi katika shule ya Kiyahudi mjini Toulouse kusini mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje, Alain Juppe anatarajiwa kuhudhuria mazishi ya watoto hao pamoja na mwalimu wao nchini Israel.

Polisi nchini Ufaransa wanaendeleza msako dhidi ya mtu aliyewaftwatulia risasi watoto hao watatu na rais Sarkzoy ameamuru maeno ya Kusini mwa nchi hiyo kuwa katika hali ya tahadhari kutokana na kile kinachoelezwa kuwa tishio la kigaidi.

Zaidi ya polisi 100 wamesambazwa katika maeneo mbalimbali Kusini mwa nchi hiyo kuendeleza msako huo.

Serikali ya Ufaransa imetangaza mauji hayo kuwa janga la kitaifa,na wanafunzi nchini Ufaransa wamesalia kimya kwa dakika moja kuwakumbuka wenzao waliouawa.

Mauji hayo pia yameshtumiwa vikali na umoja wa mataifa pamoja na Israel kupitia kwa Waziri wake Mkuu Benjamin Netanyahu.

Hata hivyo,rais Sarkzoy amewahakikishia viongozi wa Kiyahudi nchini Ufaransa kuwa serikali yake inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa tukio lingine kama hilo halitokei tena na kuongeza kuwa usalama umeimarishwa katika shule zote za kidini nchini humo.

Waziri wa maswala ya ndani Claude Gueant amesema atasalia katika mji huo wa Toulouse hadi pale,kiini cha shambulizi hilo kitakapobainika,na amesema uchunguzi wa kijasusi umebaini kuwa muuwaji huyo alikuwa na picha shingoni wakati akitekeleza mauji hayo.

Watoto hao waliouawa walikuwa na umri wa miaka mitatu,sita na kumi pamoja na mwalimu wao mwenye umri wa miaka 30 aliyekuwa anafunza somo la dini katika shule hiyo ya Ozar Hatorah.

Walioshudia kisa hicho wanasema mtu aliyetekeza mauji hayo awasili katika shule hiyo akiwa na bastola mbili akiwa juu ya pikipiki na kuanza kufwatua risasi kiholela.

Wiki iliyopita,wanajeshi watatu wa Ufaransa waliuawa Kusini mwa nchi hiyo baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.