Pata taarifa kuu
UFARANSA

Watu wanne wakiwemo watoto watatu wauawa baada ya kupigwa risasi katika shule ya Kiyahudi Kusini mwa Ufaransa

Watu wanne wakiwemo watoto watatu wameuawa Kusini Magharibi mwa Ufaransa katika mji wa Toulouse baada ya mtu mmoja aliyejihami kwa bastola kuvamia shule ya Kiyahudi.

Mauaji katika shule ya Kiyahudi Kusini mwa Ufaransa
Mauaji katika shule ya Kiyahudi Kusini mwa Ufaransa
Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia kisa hicho wanasema mtu huyo aliyekuwa na bastola aliingia ndani ya shule hiyo akiwa juu ya pikipiki na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Watu wengine wawili wanaripotiwa kujeruhiwa katika shambulizi hilo katika  shule hiyo ya Kiyahudi ya Ozar Hatorah, na polisi wanasema wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha shambulizi hilo na pia kumsakata mtu huyo.
 

Mauaji haya yanayotokea siku kadhaa baada ya wanajeshi watatu wa Ufaransa kuuawa kwa kupigwa risasi Kusini mwa nchi hiyo.

Rais Nicolas Sarkozy na waziri wa elimu,wamezuru shule hiyo na tayari rais Sarkozy amenukulia akisema ni mapema mno kubaini ikiwa mauji hayo yametokea kutokana na kuuawa kwa wanajeshi watatu  wiki iliyopita.

Usalama umeimarishwa katika majengo ya kidini na taasisi  za kidini baada ya shambulizi hilo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.