Pata taarifa kuu
UFARANSA

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ashtumu mauji yaliyotokea katika shule ya Kiyayudi,asema ni janga la kitaifa

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkzoy amesema mauji yalitokea katika shule ya Kiyayudi Kusini mwa nchi hiyo na kusabibisha kuuawa kwa watu wanne wakiwemo watoto watatu ni janga la kitaifa na ameahidi kuwa aliyetekeleza mauji hayo atakamatwa na kukumbana na mkono wa sheria.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkzoy akizungumza na waandishi wa habari
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkzoy akizungumza na waandishi wa habari Reuters / Eric Feferberg
Matangazo ya kibiashara

Akiwa katika shule hiyo katika mji wa Toulouse rais Sarkozy amesema siku ya Jumanne wanafunzi watasalia kimya kwa dakika moja kuwakumba wenzao waliouawa.

Aidha Sarkosy amewahakikishia viongozi wa Kiyahudi nchini Ufaransa kuwa serikali yake inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa tukio lingine kama hilo halitokei tena na kuongeza kuwa usalama umeimarishwa katika shule zote za kidini nchini humo.

Waziri wa maswala ya ndani Claude Gueant amesema atasalia katika mji huo wa Toulouse hadi pale,kiini cha shambulizi hilo kitakapobainika.

Watoto hao waliouawa walikuwa na umri wa miaka mitatu,sita na kumi pamoja na mwalimu wao mwenye umri wa miaka 30 aliyekuwa anafunza somo la dini katika shule hiyo ya Ozar Hatorah.

Walioshudia kisa hicho wanasema mtu aliyetekeza mauji hayo awasili katika shule hiyo akiwa na bastola mbili akiwa juu ya pikipiki na kuanza kufwatua risasi kiholela.

Wiki iliyopita,wanajeshi watatu wa Ufaransa waliuawa Kusini mwa nchi hiyo baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.