Pata taarifa kuu
Malawi

Makundi ya Wanaharakati nchini Malawi wadai kujiuzulu kwa Rais Bingu wa Mutharika

Jeshi la Polisi nchini Malawi wamefanya Doria hii leo baada ya Makundi ya Wanaharakati kumtaka Rais wa Nchi hiyo, Bingu wa Mutharika Kujiuzulu.

Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika
Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika en.wikipidea
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Davie Chingwalu ameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa wameimarisha Doria na kwamba walikuwa na Taarifa za kuwepo kwa Maandamano.

Kamati ya Maswala ya Jamii, Kundi la viongozi wa Dini na Wanaharakati wametishia kutotii ikiwa Mutharika hataachia ngazi ndani ya Siku 60 au kuitisha Kura za Maoni juu ya Uongozi wake ndani ya Miezi mitatu.

Lakini waziri wa Habari wa nchi hiyo, Patrcia Kaliati ameonya kuwa Serikali haitakaa kimya kuona Watu wakiiingiza nchi hiyo katika Vurumai na Machafuko

Utawala wa awamu ya pili wa Mutharika umeonekana kutoridhisha,hasa baada ya kuwepo msuguano wa kisiasa ulioibuka baada ya Maandamano ya Mwezi July Mwaka Jana,ambapo watu 19 waliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi, hali kadhalika kukoma kwa misaada kutoka kwa Mataifa ya kigeni kufuatia hali ya Kidemokrasia iliyopo nchini humo, utawala na namna Suala la kutetereka kwa Uchumi linavyoshughulikiwa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.