Pata taarifa kuu
MISRI-MAREKANI-PAKISTAN

Vyombo Vya Usalama nchini Misri vyakanusha aliyekamatwa kuwa si Kiongozi wa Al Qaeda Seif Al Adel

Vyombo vya Usalama Nchini Misri vimekanusha mtu ambaye amekamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Cairo kuwa si Seif Al Adel ambaye anatajwa kuwa ni Kiongozi wa Mtandao wa Kigaidi wa Al Qaeda bali ni mtu ambaye alikuwa anasakwa na serikali ya taifa hilo.

Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Seif Al Adel ambaye amekuwa akitafutwa tangu mwaka 1998 kwa kitita cha dola milioni 5
Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Seif Al Adel ambaye amekuwa akitafutwa tangu mwaka 1998 kwa kitita cha dola milioni 5
Matangazo ya kibiashara

Chanzo cha habari kutoka Vyombo vya Usalama nchini Misri kimekanusha vikali kumkamata Al Adel kama taarifa za awali zilivyokuwa zinaeleza zikimtaja kuwa mmoja wa watu wanaosakwa kwa udi na uvumba na Polisi wa Marekani FBI.

Mtu ambaye alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Cairo alikuwa anatoka Pakistan kabla ya kupitia Dubai na hivyo wengi kuhusi kuwa ni Al Adel ambaye anasakwa kwa muda mrefu sasa.

Vyombo vya Usalama nchini Misri vimesema kuwa wao wamemkamata mtu ambaye anahusishwa na makundi ya kupigania vita vya kiislam maarufu kama Al Jihad ambaye amekuwa mstari wa mbele kupanga mashambulizi.

Kauli ya kukanusha aliyekamatwa kuwa si Al Adel imekuja saa kadhaa baada ya Kituo Cha Televisheni nchini Misri kutakangazwa aliyekamatwa kuwa ni Seif Al Adel ambaye anasakwa na zawadi atakayempata kuwa ni dola milioni tano.

Taarifa za awali zilikuwa zinamhusisha mtu aliyekamatwa kuwa ni Mohummad Ibrahim Makkawi ambaye baada ya kujiunga na Mtandao wa Al Qaeda alikuwa ni miongoni mwa walinzi wa karibu wa Marehemu Osama Bin Laden.

Kabla ya taarifa hiyo kutolewa tayari wachambuzi walishakanusha kuwa aliyekematwa si Seif Al Adel kutokana na maelezo ambayo yametolewa kumuanisha yule aliyekamatwa.

Seif Al Adel anatajwa kupanga na hatimaye kutekeleza mashambulizi kwenye Balozi za Marekani katika nchi za Tanzania na Kenya na kusababisha vifo vya watu wasio na hatia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.