Ufaransa na Uingereza zasaini mkataba kuhusu nyuklia, zainyoshea kidole Syria
Ufaransa na Uingereza zimesaini mkataba wa kuendeleza ushirikiano katika masuala ya nishati ya nyuklia kwa ajili ya matumizi ya kawaida hatua ambayo inatarajiwa kusukuma maendeleo katika nchi hizo.Pamoja na kusukuma maendeleo mpango huo utasaidia kuongeza fursa zaidi za biashara zenye thamani ya Euro milioni 500 baina ya pande hizo mbili.
Imechapishwa:
Aidha mpango huo wa Ufaransa na Uingereza utaongeza nafasi za ajira kwa kutoa fursa takribani 1,500 kwa Uingereza pekee na kwamba mpango huo ni muhimu nchi husika.
Mkataba huo umesainiwa katika mkutano wa pamoja kati ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy mjini Paris nchini Ufaransa.
Rais Sarkozy anakabiliwa na kipute cha kuwania urais nchini Ufaransa Mwezi Aprili na Mei mwaka huu ambapo tayari ameshatangaza kuwania nafasi hiyo.
Viongozi hao hawakusita kuzungumzia hali ya mambo nchini Syria na wamesema ni lazima lifanyike lolote linalowezekana ili kukomesha mauaji nchini Syria.
Wametoa wito kwa dunia kuunganisha nguvu ili kuhakikisha suluhu ya kudumu inapatikana nchini Syria