Pata taarifa kuu
Pakistani

waziri mkuu wa Pakistan,Yousef Raza Gilani aitwa Mahakamani siku ya Jumatatu

Mahakama ya juu nchini Pakistan hii leo imetupilia mbali rufaa aliyoitoa Waziri mkuu wa nchi hiyo Yousuf Raza Gilani na kumtaka kufika Mahakamanni siku ya Jumatatu ili kukabili mashtaka yaliyo dhidi yake. 

Waziri Mkuu wa Pakistan, Yousuf Raza Gilani
Waziri Mkuu wa Pakistan, Yousuf Raza Gilani Reuters/Mian Khursheed
Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo ikirejelea amri iliyotolewa tarehe 2 mwezi Februari ikimtaka Gilani kufika Mahakamani kujibu shutma za kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Rais wa nchi hiyo Asif Ali Zardari anayeshutumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Ikiwa Gilani atathibitishwa kuwa na hatia, atatumikia kifungo mpaka cha miezi sita Jela na kusimamishwa wasdhifa wake wa Uwaziri Mkuu kufuatia Kesi hiyo ambayo wakosoaji wanatarajia kuongeza shinikizo kwa Serikali kuitisha mapema uchaguzi miezi michache ijayo.

Zardari na Marehemu Mkewe, Benazir Bhuto walikuwa wakishukiwa kutumia akaunti za Benki ya Uswisi kujitwalia fedha isivyo, ikiwa ni rushwa kutoka kwa Makampuni yaliyokuwa yakisaka kupatiwa mikataba ihusuyo maswala ya Ushuru wa Forodha miaka ya 1990

Jaji Mkuu wa Mahakama hiyo Iftikhar Muhammad Chaudry amesema Mahakama itaachana na amri hiyo ikiwa Gilani atatii amri ya kuandikia mamlaka ya Uswisi kuitaka ifungue tena kesi iliyokuwa imefungwa zaidi ya miaka miwili nyuma.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.