Pata taarifa kuu
Ulaya

Nchi za Ulaya kukabiliwa na hali ngumu zaidi ya kiuchumi

Taasisi ya kutathmini viwango vya uchumi duniani ya S and P imeonya kuwa huendsa hali ya kiuchumi ikawa mbaya zaidi barani Ulaya ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa. Onyo hilo la taasisi hiyo linakuja huku viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wakiwa katika mstari wa mbele kushughulikia hatari hiyo ya madeni na kuporomoka kwa uchumo katika bara hilo.

REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na taasisi hiyo, inakisiwa kuwa viwango vya kiuchumi huenda vikashuka kwa asilimia hamsini kama hatua madhubuti hazitachukuliwa ili kukabiliana na hali hiyo.

Kwa sasa tajamani ya sarafu ya Euro imeshuka pamoja na kupunguka kwa baishara katika masoko ya hisa baranai ulaya.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy na Kansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel wanasema kuwa mkataba mpya baina ya mataifa yanayotumia sarafu ya Euro, unastahili kubuniwa ili kukabaliana na hali ngumu ya uchumi katika bara hilo kwa sasa.

Siku ya Ijumaa wiki hii viongozi wa mataifa 17 sarafu ya Euro wanatarajiwa kukutana Brussles Ubelgiji kujadili mapendkezo hayo ya Ufarsasa na Ujerumani, ambao viongozi hao wanasema ni kujaribu keleta nidhamu katika masuala ya mikopo kwa mataifa yanayotumai sarafu ya Euro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.