Pata taarifa kuu
Afghanistan

Karzai ahitaji mchango wa jumuiya ya kimataifa hata baada ya mwaka 2014

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai amesema kuwa mchango wa jumuiya ya kimataifa utaendelea kuwa muhimu kwa nchi yake hata baada ya kuondoka kwa majeshi ya kigeni yaliyoko nchini humo.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Hamid Karzai amesema kuwa mchango huo wa jumuiya ya kimataifa haupaswi kukoma kama kweli jumuiya hiyo inataka Afghanistan isimame imara bila kutetereka.

Karzai ametoa changamoto hiyo mjini Bonn nchini Ujerumani katika mkutano wa kimataifa wa kuangalia hali ya baadaye ya Afganistan.

Mkutano kama huo uliwahi kufanyika miaka kumi iliyopita baada ya kundi la Taliban kuangushwa.

Kutokana na hali ilivyo nchini Afghanistan, majeshi yan kigeni yamekuwa yakisaidiana na majeshi ya serikali kukabiliana na vikundi vya kigaidi likiwemo kundi la Taliban hali ambayo imekuwa tishio kwa usalama wa raia.

Majeshi ya kigeni yaliyoko nchini Afghanistan yanatarajiwa kuondoka nchini humo ifikapo mwaka 2014 na kuyaacha majeshi ya seikali yakiendelea na jukumu la kulinda usalama wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.