Pata taarifa kuu
Syria

Muungano wa nchi za kiarabu waorodhesha vikwazo dhidi ya serikali ya Syria.

Mawaziri wa fedha kutoka muungano wa nchi za kiarabu wameorodhesha vikwazo dhidi ya rais Bashar Al Asaad wa Syria pamoja na viongozi wengine katika serikali yake baada ya Syria ,kukataa kukubali waangalizi kutoka umoja huo kuzuru nchi hiyo ili kuchunguza mauji dhidi ya waandamanaji,yanayoendelea.

Mawaziri wa fedha wa nchi za kiarabu wakiwa Cairo Misri
Mawaziri wa fedha wa nchi za kiarabu wakiwa Cairo Misri (REUTERS)
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa vikwazo hivyo vilivyoafikiwa na mawaziri hao ni pamoja na kuwazuia viongozi wa serikali ya rais Asaad kuzuru taifa lolote la kiarabu pamoja na kustaafisha mali ya serikali iliyowekezwa katika mataifa mbalimbali ya muungano huo.
 

Kikwazo kingine ni pamoja na kusitisha safari za ndege kutoka Syria kwenda katika mataifa ya kiarabu pamoja na kusimamisha huduma zozote na benki kuu ya Syria,pamoja na kusitisha miradi yeyote ya maendeleo kutoka kwa muungano huo nchini Syria.
 

Hata hivyo waziri wa nchi za kigeni wa Syria Walid Muallem amekashifu vikwazo hivyo vya mataifa hayo 22 na kudai kuwa yanashirikiana na nchi za magharibi,kuendeleza machafuko nchini mwake.
 

Aidha serikali hiyo ya Damascus inadai kuwa wangalizi kutoka mataifa hayo ya kiarabu wanalenga kuendeleza ubabe wa nchi za magharibi nchini Syria badala ya kuwaachia wananchi wa Syria kutatua matatizo yao wenyewe.
 

Shinikizo zinazidi kutolewa kwa rais Bashar Al-Asaad  kujiuzulu na kukomesha mauji dhidi ya waandamanaji.
 

Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya watu elfu 3 wameuawa mikononi mwa wanajeshi wa Syria tangu maandamano dhidi ya rais Bashar Al Asaad yalipoanza mapema mwaka huu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.